HABARI MOTO MOTO ...

Friday, May 2, 2014

`Serikali iunge mkono mpango wa kupunguza athari dawa za kulevya`


Serikali imetakiwa kutekeleza na kuunga mkono mpango wa kupunguza madhara hasi yanayohusiana na matumizi ya dawa za kulevya pamoja na kurejesha maisha bora katika jamii. Hayo yalisemwa Dar es Salaam na Greg Denham, Mratibu katika Mtandao wa Kimataifa wa Utekelezaji Sheria na VVU (LEAHN) alipotembelea Mtandao wa Watu wanaotumia dawa ya kulevya nchini (TaNPUD) na Ofisi za Madakitari wa Ulimwengu (MdM).

Monday, January 27, 2014

PROF. BEREGU AFICHUA SIRI NZITO NDANI YA CHADEMA..AWEKA WAZI KIINI CHA USALITI NDANI YA CHAMA HICHO..SOMA ZAIDI KUJUA UKWELI

MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Profesa Mwesiga Baregu, amefichua siri ya madai ya usaliti ndani ya chama hicho. Akizungumza na Mtanzania katika mahojiano maalumu yaliyofanyika jijini Dar es Salaam wiki hii, Profesa Baregu alisema kiini cha tuhuma na madai ya usaliti ndani ya Chadema ni kutoaminiana na kukosekana kwa uvumilivu. Alisema kitendo cha wanachama na viongozi kunyoosheana vidole vya usaliti kinakiangusha chama na kwamba Chadema kimefeli katika mambo matatu, ambayo ndiyo yanapaswa kuwa msingi wa chama na kama yangezingatiwa mapema, hoja ya usaliti isingezungumzwa leo. Aliyataja mambo hayo yanayozalisha hoja nzito ya usaliti iliyosababisha baadhi ya wanachama wa chama hicho kuvuliwa uanachama kuwa ni kusikilizana, kuvumiliana na kuaminiana. “Kukosekana kwa mambo hayo ndio kiini cha kuibuka kwa hoja ya usaliti, hatua hii ni mbaya katika maendeleo ya chama kinachojijengea uaminifu kwa wananchi,” alisema.

DOWNLOAD 20 PERCENT - SUBIRA

Sunday, January 26, 2014

Mfuko wa Rais wakumbwa na kashfa

Mfuko  wa Rais wa Kujitegemea (PTF) umekumbwa na kashfa nyingine baada ya kudaiwa kuwadhulumu wanachama wake akiba zenye thamani ya zaidi ya milioni 10/-.
Wanachama hao ambao ni kikundi cha Mbezi A na B wamedai kuwa mpaka sasa imeshapita miaka mitatu wamekuwa wakipigwa kalenda kila wakati kuwa watapatiwa akiba zao jambo ambalo limeshindikana kutekelezeka.

Saturday, January 25, 2014

Mwanamke wa miaka 48 , mkazi wa Rombo akamatwa na polisi kwa kufanya ngono na watoto wa miaka 9- 14 kwa zamu.....

Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Aretas Joseph, (48), mkazi wa kijiji cha Lesoroma tarafa ya Useri, wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro, amehojiwa na polisi mkoani hapa kwa tuhuma za kufanya mapenzi na watoto wadogo wa kiume, wenye umri kati ya miaka 9 na miaka 14, jambo linaloelezwa kuwa ni shambulizi la aibu.

KASHFA YA KUSAGANA KATI YA IRENE UWOYA NA MARIAM....YAWA GUMZO MITANDAONI UKWELI HUU HAPA..

                                                               Mariam IsmailMastaa wa filamu nchini Mariam Ismail na Irene Uwoya wanadaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi(usagaji) na kudaiwa kuishi pamoja kabisa. wiki kadhaa nyuma muigizaji mmoja chipukizi anayekuja juu kwa kasi aliutonya mtandao huu kwa kusema " Mariam Ismail na Uwoya wanasagana tena wanaishi pamoja kabisa, fuatilieni mtajua".

Sunday, October 27, 2013

cheki picha ...AJALI MBAYA YATOKEA MBEZI JIJINI DAR, BAADA YA DALADALA KUGONGA MAGARI 2 NA BAJAJI 2

Ajali mbaya imetokea eneo la bondeni, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam baada ya daladala ya Mwenge Kariakoo kukosa break na kugonga magari mawili na bajaji mbili. Katika ajali hiyo mama mmoja amegongwa vibaya na amekimbizwa hospitali ya Lugalo kwa matibabu.
                      Hali haikuwa nzuri maana kila mmoja alikuwa katika hali ya taharuki.
                                                Bajaji zikiwa zimegongwa vibaya