HABARI MOTO MOTO ...
Wednesday, October 31, 2012
MBEYA.
Mnamo tarehe 29-10-2012 majira ya saa10 jioni katika kijiji cha Mkola wilayani Mbozi mkoani Mbeya,askari polisi wakiwa katika dolia walimkamata Kaogoma Christopher Kashola (20,Mfipa,mkulima mkazi wa kijiji cha Mtanila akiwa na bangi debe 8 ikiwa ni sawa na kilo 25.
Bangi hiyo alikuwa ameificha ndani ya nyumba yake huku mtuhumiwa huyo akiwa ni muuzaji na pia ni mvutaji wa bangi na sasa yupo mahabusu na taratibu za kumfikisha mahakamani zinaendelea.
Alithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya kamishna msaidiziwa polisi Diwani Athumani alitoa wito kwa jamii kujiepusha na matumizi ya dawa za kulevya kwani ni hatari kwa afya zao nani kinyume na sheria.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment