Wapinganaji hao wastaafu wametapeliwa
mamilioni ya fedha zikiwemo ada za uanachama za kujiunga na muungano wao
pamoja na fedha za gharama za kuanzisha vikundi vya wajasiriamali
katika kupambana na ukali wa maisha baada ya kumaliza utumishi wa umma.
Hayo yamefahamika katika mkutano wa
wanachama wa Muungano huo kutoka Mikoa mitano ya Zanzibar uliyofanyika
Amani, Mkoa wa mjini Magharibi Kisiwani Unguja na kuhudhuriwa na
Mwenyekiti wa muda wa Muwawata, Brigedia Jenerali Mstaafu Haroun
Othmani.
Akisoma azimio la mkutano huo, Mwenyekiti
wa Muwawata, Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Sajenti Mstaafu wa JWTZ
Miraji Kiongwe, alisema wanaunga mkono kuondolewa madarakani kwa Sajuni
Taji mstaafu Mayugi kutokana na tuhuma za ubadhirifu wa fedha za
muungano huo.
“Mikoa mitano ya Zanzibar kama wanachama
tunaunga aliyekuwa Mwenyekiti wetu Asseyd Mayungi kuondolewa uongozi kwa
tuhuma za kuhusika na ubadhirifu wa fedha za Muwawata,” alisema
Kiongwe.
Alisema baada ya wanachama kujadili kwa
kina ripoti ya ubadhirifu wa fedha za Muwawata wamekubaliana kila
kikundi cha ushirika kilichotapeliwa fedha kufungua kesi haraka dhidi ya
Mayungi na watu alioshirikiana nao kufanikisha mpango huo.
Kiongwe alisema Mayungi anatuhumiwa
kuzunguka katika mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na Zanzibar na
kukusanya mamilioni ya fedha kama ada za kujiunga na Muwawata pamoja na
fedha za kusajili vikundi vya Ushirika vya askari wastaafu kabla ya
kupatiwa mikopo.
Alisema kwamba kazi hiyo alikuwa akiifanya
kwa kushirikiana na Taasisi moja ya kusadia Wajasiriamali (jina lake
linahifadhiwa) ambao walifika Zanzibar na kufanikiwa kukusanya fedha
kutoka vikundi 18 vya ushirika.
Alisema Mayungi kwa kushirikiana na
Taasisi hiyo jumla ya Sh. 23,880,000 zimekusanywa na kutumika tofauti
na malengo ya Muwawata.
Kiongwe alisema kwamba tangu kukusanywa
fedha hizo mwaka jana wamekuwa wakifuatilia maendeleo ya mikopo bila ya
mafanikio kwa Taasisi hiyo ya kusaidia wajasiriamali na kubainika kuwa
tayari wametapeliwa.
Akizungumza katika mkutano huo Mwenyekiti
wa Kamati ya mpito ya Uongozi wa Muwawata, Brigedia Jenerali Mstaafu
Othman, aliwataka wanachama wa Muungano huo kuwa na moyo wa subira
wakati tatizo hilo likishughulikiwa na uongozi wa mpito kabla ya
wahusika kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Hata hivyo aliwataka kuendelea kuunga
mkono viongozi walichaguliwa kwa muda kuongozi ili kuhakikisha malengo
ya kuanzishwa kwa Muungano huo yanafanikiwa na kuwanufaisha wanachama
wake.
Juhudi za kuwapata Asseyd na Taasisi ya
kusaidia wajasiriamali ambazo zimekubwa na kashfa ya kuwatapeli wastaafu
hao wa JWTZ hazikuweza kuifanikiwa kupitia simu zao za na barua pepe.
No comments:
Post a Comment