ZAIDI ya robo tatu ya wanafunzi katika shule za msingi wilayani
Maswa, mkoa wa Simiyu, hushinda bila kupata mlo wa mchana wala maji ya
kunywa wawapo shuleni na kusababisha kiwango cha ufaulu kushuka.
Tatizo hilohilo pia huwakumba walimu wa shule hizo kutokana na kuishi mbali na makazi yao kutokana na shule nyingi kutokuwa na nyumba za walimu.
Hayo yalielezwa na Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Luten mstaafu Abdallah Kihato, alipokuwa akizungumzia changamoto zinazoikabili sekta ya elimu ya msingi wilayani hapa na kusababisha kuwepo kwa mdololo mkubwa wa ufaulu na kuwapo kwa wimbi kubwa la utoro.
Alisema shule nyingi wilayani humo hazina huduma ya chakula kwa wanafunzi wake na imekuwa sababu kubwa inayochangia kushuka kwa taaluma na kiwango cha utekelezaji wa mitaala na kusababisha kiwango cha utoaji wa elimu ya msingi kuwa chini ya wastani wa asilimia 50.
Kutokana na hali hiyo, aliwashauri madiwani wa halmashauri hiyo kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo kwa kuhakikisha wanafunzi wanapata angalau mlo wa mchana na majisafi wawapo shuleni.

No comments:
Post a Comment