HABARI MOTO MOTO ...

Wednesday, April 17, 2013

picha za enzi ya uhai wa marehemu BIbi Kidude.

Marehemu Bibi Kidude amekufa akiwa na miaka 105,ni mwanamuziki  mkongwe sana katika muziki wa taarabu ambapo alipata umaarufu sana bala na visiwani.viongozi wa serikali na wasanii wauzunika sana kwa kifo cha mkongwe huyu. endelea kupata taarifa zaidi

Wapinzani wa Azam watua kwa mafungu

Kundi la kwanza la wachezaji na viongozi wa timu ya AS FAR ya Morocco inayokuja kuivaa Azam katika mechi yao ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya Kombe la Shirikisho kwenye Uwanja wa Taifa  jijini Dar es Salaam Jumamosi liliwasili nchini jana mchana.

Akizungumza na NIPASHE, Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),  Boniface Wambura, alisema kuwa kundi hilo liliwasili saa 8:00  mchana kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa kundi la mwisho la kikosi hicho litatua nchini leo mchana.

Wambura aliongeza kuwa maandalizi ya mechi hiyo yako katika hatua za mwisho na wanaamini kuwa Azam watafanya vyema katika mechi hiyo na kujiwekea mazingira mazuri ya kusonga mbele kwenye mashindano hayo wakiwa ni wawakilishi pekee wa Tanzania waliobaki katika michuano ya kimataifa.

Alisema vilevile kuwa marefa wa mechi hiyo walioteuliwa kutoka Shelisheli ambao ni Emile Fred atakayepuliza filimbi akisaidiwa na Steve Maire na Jean Ernesta na wa mezani, Jean Claude Labrossa watatua nchini keshokutwa.

Alimtaja Kamishna wa mechi hiyo kuwa ni Abbas Sendyowa kutoka Uganda ambaye pia atatua nchini keshokutwa.

Azam inayoshiriki michuano hiyo ya Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) kwa mara ya kwanza, imefika hatua hiyo baada ya kuzitoa Al Nasri ya Sudan na Barrack Young Controllers ya Liberia.

Simba iliyokuwa ikiiwakilisha Tanzania katika Ligi ya Klabu Bingwa Afrika ilitolewa hatua ya awali na Recreativo de Libolo ya Angola kwa kipigo cha jumla cha mabao 5-0.