HABARI MOTO MOTO ...

Sunday, October 27, 2013

cheki picha ...AJALI MBAYA YATOKEA MBEZI JIJINI DAR, BAADA YA DALADALA KUGONGA MAGARI 2 NA BAJAJI 2

Ajali mbaya imetokea eneo la bondeni, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam baada ya daladala ya Mwenge Kariakoo kukosa break na kugonga magari mawili na bajaji mbili. Katika ajali hiyo mama mmoja amegongwa vibaya na amekimbizwa hospitali ya Lugalo kwa matibabu.
                      Hali haikuwa nzuri maana kila mmoja alikuwa katika hali ya taharuki.
                                                Bajaji zikiwa zimegongwa vibaya

Picha,Diamond Anafanya Remix Ya My Number One Na Huyu Star Kutoka Nigeria

Picha inaonyesha akiwa studio na Davido tayari kurekodi Number One Remix. Video Itakuwa na mchanganyiko wa Dance ya Ngololo Na Skelewu

habari za ivi punde... : BABA MZAZI WA MWANADADA WEMA SEPETU AFARIKI DUNIA.....

Siku chache tu baada ya kuanza kurushwa hewani kwa kipindi halisia cha televisheni(Reality Show) yake, muigizaji, mrembo maarufu nchini Tanzania (Miss Tanzania 2006),Wema A. Sepetu, amepatwa na msiba mkubwa. Amefiwa na Baba yake mzazi,Balozi Isaac Abrahamu Sepetu. Taarifa ambazo BC imezipata zinapasha kwamba Mzee Sepetu ambaye kwa muda wa miezi kadhaa sasa amekuwa akiugua na kusumbuliwa na maradhi ya kiharusi,. Mzee Sepetu alikuwa pia akisumbuliwa na kisukari.Amefariki jijini Dar-es-salaam. Mipango ya mazishi inafanyikia nyumbani kwa marehemu maeneo ya Sinza-Mori jijini Dar.

KIM KARDASHIAN NA KANYE WEST WATOA MPYA NA KALI YA MWAKA....!

Hii ni kali ya mwaka imegundulika kuwa Kanye West na Kim Kardashian wamekubaliana kusign mkataba ambao endapo wataoana kwa ndoa hivi karibuni basi kila mtu atakuwa na mali zake kivyake ili endapo wakiachana wasigawane mali jambo ambalo huleta vita sana katika mahusiano ya ndoa endapo yatavunjika.....Katika hilo watakuwa na account moja tu ya kuendesha familia ambayo watakuwa wanachangia ...Je wewe walionaje hilo ? linafaa hapa Bongo ?

DIAMOND, DAVIDO, MOHOMBI NA NAY WA MITEGO KUFANYA SHOW YA BURE LEADERS CLUB LEO SAA TISA MCHANA.

Kutokana na kutokea hitilafu ya umeme Alfajiri ya leo kwenye show ya Serengeti Fiesta Dar, iliyopelekea baadhi ya wasanii waliokuwa wakitarajia kupanda jukwaani kutumbuiza akiwemo Davido, Mohombi, Diamond, Nay wa Mitego na wengine kushindwa kupanda, leo kuanzia saa tisa, wasanii hao watapanda tena jukwaani kuzikonga nyoyo za mashabiki wao bila kiingilio chochote. Ni katika uwanja ule ule, jukwaa lile lile la Serengeti Fiesta Dar es Salaam ambapo Diamond,Davido,Mohombi pamoja na Nay wa Mitego watapanda kuanzia saa 9 jioni mpaka saa 12.Show hiyo ya bure itapambwa pia na bendi ya Twanga Pepeta.

Wednesday, October 23, 2013

YAJUE MADHARA YA KUTOKULALA KWA MUDA MREFU KWA MWANAUME

Usingizi ni dawa ambayo inaweza kukutibu bila wewe kujua, kwa hiyo inafaa uitumie mara nyingi. Ni wengi katika jamii ambao hawafahamu umuhimu wa kupata muda mzuri wa kulala katika maisha yao. Pia, wengi hawatambui jinsi ukosefu wa usingizi wa kutosha ulivyo na athari kwao na kuwa kulala kwa muda mfupi kunapunguza kichochezi dume kiitwacho testosterone Mwonekano wa mwanamume yeyote duniani na kupata sifa ya kuitwa mwanamume husababishwa na kichochezi hiki testosterone.

(Video) Muthoni The Drummer Queen - Nai Ni Ya Who

NGOMA MPYA: NIKKI MBISHI - YOTE MAISHA

Hii ni ngoma mpya kabisa ya rapper Nikki Mbishi inayoitwa "Yote Maisha". Ni moja kati ya ngoma ambazo zipo katika Kanda Mseto yake mpya ambayo aliizindua siku chache zilizo pita. Isikilize ngoma yenyewe hapa chini....

TUNDA MAN KUACHIA "MSAMBINUNGWA" HIVI KARIBUNI...

Huu ni ujio mwingine mpya kabisa kutoka kwa msanii Tunda Man kutokea TipTop Connection Manzese. Ambapo katik ujio huu wa Msambinungwa Tunda amemshirikisha AlliKiba. Kaeni tayari kwa ujio huu na pia endelea kutembelea AnnaPeter.Com ili uweze kupata kuusikiam wimbo huu hapa exclusively.

VIDEO MPYA: GODZILLA FT. WALTER CHILAMBO - THANKS GOD

"Thanks God" ni video mpya kabisa ya rapper kutoka Salasala maarufu kama Godzilla Zizi akiwa amemshirikisha msanii Walter Chilambo ambae alikuwa ni mshindi wa kwenye mashindano ya kusaka vipaji vya uimbaji Tanzania BSS. Chukua dakika zako chache za kuitazama video yenyewe hapa chini...

POLISI WAREJESHA VITITA VYA FEDHA ZA WACHINA VILIZOIBWA KATIKA TUKIO LA UTEKAJI

"Jamani pesa yenu iliyoibiwa hii hapa," Ni kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Iringa ACP Athmani Mungi akiwaonyesha raia wa China maburungutu ya fedha zilizonusurika kutoka kwa majambazi waliowateka na kuwapora raia wa China.
Fedha shilingi Milioni 80 ambazo zimerejeshwa na jeshi la polisi kutoka mikononi wa majambazi wa tukio la utekaji wa raia wa Kichina, waliovamiwa katika mlima wa Nyang'olo mkoani Iringa.

Tuesday, October 22, 2013

JK 'MSALITI MJENZI' AVIWEKA VYAMA VYA SIASA PAMOJA, SASA MUSWADA KURUDIWA

Viongozi wa vyama vya Siasa,(kushoto)Isaack Cheyo(UDP), Nancy Mrikaria (TLP), Fahmi Nassoro Dovutwa (UPDP), James Mbatia NCCR-Mageuzi, Profesa Ibrahim Lipumba (CUF), Philip Mangula (CCM) na Dk Willibrod Slaa (Chadema) wakiwa wameshikana mikono baada ya kikao cha pamoja jijini Dar es Salaam jana.

Monday, October 21, 2013

Mr Blue Aelezea sababu za Yeye kutoonekana kwenye Video Ya Hemedy- Rest Of My Life

Mr Blue ameeleza Kuhusu sababu za kupotezea video ya Hemedy Phd - Rest Of My Life iliyotoka Ijumaa. Blue amesema "Ni kweli Hemedy alinitafuta tufanye video ila wakati huo nilikuwa na show nje ya nchi na nilivyo rudi sikuwa na nafasi ila tulikubaliana kuwa tuta shoot hivi karibuni, Blue amendelea kusema Ameshangaa sana kusikia kuwa video imetoka bila yeye kuwepo na kuwa Hemedy amechana mistari yake, Sina sababu ya kutokuwepo kwenye video ya Hemedy kwani sisi ni marafiki na nampa heshima sana Hemedy kama kaka yangu, Nikimuona Hemedy nitamuliza kwanini ameshindwa kusubiri mpaka niwe na muda wa kufanya sehemu yangu na ametoa video bila mimi"

SIKILIZA NA DOWNLOAD TRACK YAO MPYA "SIRI YA MCHEZO"- FID Q ft. JUMA NATURE...!

JUSTINE BIEBER AANZA MCHEZO MBAYA.....!

Mastaa wengi wa dunia wamewahi kuonekana kwenye matukio ya kuwa karibu na stripper ambapo miongoni mwao ni Ne-yo ambae hiki kitendo kiliwahi kumpa lawama nyingi na sio pongezi, hii ni kutokana na picha waliyokua nayo mashabiki juu yake kwamba ni miongoni mwa mastaa wastaarabu wasiotaka sifa ambao huwezi kuwaona wakichezea hela na kuzirusha kwenye mwili wa stripper.

LICHA YA MATISHIO YA UGAIDI: Mlimani City yasitisha ukaguzi wa Magari na watu kwa madai kwamba unapunguza wateja!

Siku chache baada ya kuanzisha ukaguzi wa magari na watu wanaoingia katika maduka ya Mlimani City, ukaguzi huo sasa umesitishwa. Hatua hiyo ilifuatia tishio la ugaidi baada ya duka la Westgate la Nairobi nchini Kenya kushambuliwa na kikundi cha Al-shabab na kusababisha mauaji ya watu 68 na wengi kujeruhiwa.

HABARI PICHA: AJALI MBAYA ILIYOTOKEA JANA MKOANI MBEYA ..

GARI AINA YA SUZUKI NA NISSAN ZIMEGONGANA USO KWA USO MAENEO YA IWAMBI JIJINI MBEYA MCHANA WA LEO KISA CHA AJALI HIYO MAPAKA SASA HAKIJAJULIKANA
HAPA BAADHI YA WANANCHI WAKIJARIBU KUYANASUA MAGARI HAYO

Soggy Doggy Ft.Abbas Kubaff & Ukoo flani Maumau_Haina jina

Linex - Kimugina

Kimugina ndio jina la ngoma hii kali kutoka kwa msanii Linex Mjeda ambae weekend hii iliyoisha siku ya jumamosi ndio alizindua video hii. Na we chukua dakika zako chache za kuweza kuitazama video hii ya Kimugina hapa chini...

Boko Haram waua madereva 19 Nigeria

Wanamgambo waliokuwa wamevaa nguo za kijeshi, wamewaua watu 19 katika kuzuizi cha barabarani walichokuwa wameweka kukagua magari katika jimbo la Borno.
Wanaume hao waliokuwa wamejihami , waliwasimamisha madereva na kuwaamrisha kuondoka kutoka katika magari yao kabla ya kuwapiga risasi na kuwaua.
Walioshuhudia tukio hilo waliambia BBC kuwa wanaume hao walikuwa wanachama wa Boko Haram, ingawa kundi hilo bado halijatamka chochote kuhusu mauaji hayo.
Jimbo hilo la Kaskazini mwa Nigeria liko chini ya sharia ya hali ya hatari, huku Boko Haram wakiwa vitani na serikali kutaka utawala wa kiisilamu.
Kundi hilo huwalenga raia na wanajeshi kwa mashambulizi ikiwemo shule na makabiliano ya mara kwa mara na jeshi la taifa.
Shambulizi la hivi karibuni, lilifanyika Jumapili, asubuhi karibu na mji wa Logumani, ambao hauko mbali sana na mpaka na Cameroon.
Walionusurika shambulizi hilo walisema kuwa washambuliaji walivaa nguo za jeshi na walikuwa wanaendesha pikipiki kabla ya kuwashambulia waathiriwa.
"Takriban wanaume 9 walituamuru kuondoka kwenye magari yeu na kulala chini,’’ alisema mwanamume
"Waliwaua watu 5 kwa kuwapiga risasi na kasha kuwanyonga wengine 14 kabla ya mtu mmoja kuwapigia simu na kuwambia kuwa wanjeshi wanakuja.’’
Alisema washambuliaji baadaye walitoroka na kujificha msituni kwa pikipiki zao.
Manusura mwingine alisema kuwa alisikia mtu aliyekuwa karibu naye akiuawa kwa kisu. Alisema ana uhakika kuwa washambuliaji walikuwa Boko Haram kwa sababu ya kuwa na ndevu.
Mwandishi wa BBC Tomi Oladipo alisema kuwa ni jambo la kawida kwa polisi kuweka vizuizi barabarani hasa katika maeneo yenye misukosuko na huenda washambuliaji waliiga mbinu hioyo ya jeshi ili kuwanasa waathiriwa. I,
Boko Haram limezua mgogoro mkubwa wa kisiasa Nigeria tangu mwaka 2009, nia yao kuu ikiwa kuunda utawala wa kiisilamu, hasa katika maeneo ya kaskazini mwa nchi
Kundi hilo limelaumiwa kwa mashambulizi kadhaa ambao yamesababisha takribna vifo 2,000 tangu mwka 2011.

`Uncle J` hatunaye

Aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Radio One, Julius Nyaisanga (53), maarufu kama ‘Uncle J’ amefariki dunia. Nyaisanga alifariki jana asubuhi katika Hospitali ya Mazimbu, mjini Morogoro baada ya kuugua ugonjwa wa kisukari na shinikizo la damu matatizo yaliyokuwa yakimsumbua kwa muda mrefu. Mtangazaji huyo maarufu na mkongwe nchini mauti yamemkuta akiwa Meneja Mkuu wa Abood Media. Akizungumza na waandishi wa habari jana, Meneja Matangazo wa Abood Media, Abed Dogoli, alisema alipokea taarifa ya kifo cha Nyaisanga jana asubuhi na kusema alifariki dunia jana hiyo majira ya saa 1:00 asubuhi katika Hospitali ya Mazimbu, iliyopo Manispaa ya Morogoro. Alisema taratibu za mazishi zinafanyika nyumbani kwa marehemu eneo la Kihonda, mjini hapa. Alisema wanatarajia kumsafirisha kwenda nyumbani kwao mkoani Mara kwa maziko na kwamba, taarifa zaidi zitatolewa kama kutakuwa na mabadiliko. Hata hivyo hakusema mazishi hayo yatafanyika lini. Kwa upande wake, Mke wa marehemu, Leah Nyaisanga, alisema enzi ya uhai wake, mumewe aliwahi kufanya kazi Radio Tanzania (RTD), pia aliwahi kufanyakazi IPP Media akiwa kama mtangazaji Radio One na baadae alipandishwa cheo hadi kuwa Mkurugenzi wa radio hiyo. Alisema marehemu pia aliwahi kufanya kazi Radio Deutsche Welle ( DW) ya nchini Ujerumani. Kwa mujibu wa Leah, mumewe pia aliwahi kwenda katika nchi za Marekani, Japan na Ghana kwa kazi za habari. .Alisema juzi jioni, hali ya mumewe ilibadilika ghafla na kuzidiwa na kukimbizwa Hospitali ya Mazimbu, Manispaa ya Morogoro, na kwamba, alifikwa na umauti jana asubuhi. Marehemu Nyaisanga ameacha mke mmoja na watoto watatu, ambao ni Samuel, Noela na Beatrice. Mbunge wa Morogoro Mjini (CCM), Aziz Abood, ambaye familia yake ndiyo wamiliki wa Kituo cha Abood Media alisema amepokea kwa masikitiko makubwa msiba wa Nyaisanga akimwelezea kuwa alikuwa mchapakazi hodari. Alisema alimfahamu Nyaisanga miaka mingi tangu akiwa katika vituo mbalimbali vya utangazaji na alikuwa mahiri katika utangazaji na maarufu. Kabla ya kwenda Aboud Media, Nyaisanga alikuwa Mkurugenzi wa Radio One akiwa ni mmoja wa watangazaji waanzilishi wa radio hiyo akitokea Radio Tanzania (RTD). Nyaisanga atakumbukwa kwa sauti yake nzuri na utangazaji wake mahiri, ucheshi na kupenda kushirikiana na watu wengine.

Sunday, October 20, 2013

Yanga na Simba zatoka sare ya mabao 3 -- 3 ligi kuu Tanzania bara.

SIMBA, YANGA WAGAWANA VIPINDI TAIFA, NGASSA AOKOA NYUMBA ZAKE APIGA BAO

Mshambuliaji wa Yanga Hamis Kiiza akifunga bao la pili katika mchezo huo huku Haruna Shamte na kipa Abel Dhaira wakiwa wameduwaa SIMBA imeonyesha kuwa bado ni wababe katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kulazimisha sare wakiwa nyuma ya mabao 3-0 dhidi ya wapinzani wao Yanga katika mchezo wa ligi hiyo uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Katika mchezo huo ambao ulihudhuriwa na mashabiki lukuki kiasi cha kuuzaja uwanja huo, Simba walijikuta wakienda vyumbani wakiwa tayari wamekubali kipigo cha mabao matatu huku wakiwaaacha Yanga wakitawala mchezo kwa kipindi chote cha kwanza. Yanga ambao walianza mchezo huo kwa kasi walipata mabao yao kupitia kwa Mrisho Ngassa ambaye alitangaza kuchoma nyumba zake tano kama hatafunga bao katika mchezo huo au kutoa pasi ya bao, hivyo kwa bao hilo ameokoa nyumba zake. Mabao mengine mawili ya Yanga yalifungwa na Mganda, Hamis Kiiza akimalizia kazi nzuri za Didier Kavumbagu ambaye alimtengenezea mabao yote mawili. Mashabiki wa Yanga walijua tayari wamemaliza kazi kwaki timu yao ilikuwa ikicheza soka safi huku wakiwa mbele kwa mabao matatu, lakini kibao kiligeuka na wapinzani wao kurudi kwa kutawala kipindi cha pili na kusawazisha mabo yote mawili.
Beki wa Simba, Joseph Owino akiwa makini kuhakikisha Mrisho Ngassa asilete madhara langoni mwao Mabao ya Simba katika mchezo huo yalifungwa na Betrum Mombeki, Said Hamis kabla ya Gilbert Kaze kuwaahamsha mashabiki wa Simba ambao waliamini kuwa wamelala katika mchezo huo. Simba: Abel Dhaira, Said Nassor, Haruna Shamte, Gilbert Kaze, Joseph Owino, Jonas Mkude, Ramadhani Singano, Abdulhalim Humud/Said Hamis, Betrum Mombeki, Amis Tambwe na Haruna Chanongo/Willium Lucian. Yanga: Ali Mustafa, Mbuyu Twite, David Luhende, Nadir Haroub, Kelvin Yondani, Athuman Idd, Haruna Niyonzima, Frank Domayo, Didier Kavumbagu, Mrisho Ngassa na Hamis Kiiza/ Simon Msuva

Saturday, October 19, 2013

PHD FT MR BLUE - REST OF MY LIFE OFFICIAL VIDEO

YOUNG DEE AKANUSHA SKENDO YA KUTUMIA MADAWA YA KULEVYA

Msanii Young Dee amekanusha uvumi ulioenea mitaani kuwa anajihusisha na matumizi ya dawa za kulevya na kusema kuwa pamoja na story hizo kuwa kubwa lakini hali hiyo haijamuathiri sana kwasababu hazina ukweli wowote.

“Ni story ambazo zimekuwa kubwa sana lakini hazijaniathiri sana kwasababu sio ukweli, lakini zimenifanya nimezidi kuwa makini sana kuwa muoga pia na vitu vingi sana kuangalia watu wanaonizunguka, mazingira na vitu kama hivyo”.
Alisema Young Dar es salaam kupitia E-News ya EATV jana . 
Dee amesema kuwa anafahamu fika kuwa utumiaji wa ‘unga’ unaweza kuathiri kazi yake ya muziki kutokana na mifano hai ambayo imeshaonekana kwa wasanii wengine, 
“The more the story zinakuwa kubwa zinapoteza maana nzima ya kitu nachohangaikia kila siku ambayo ni muziki, so naonekana muziki nafanya nakula unga na mifano ipo watu ambao wameingia kitika hayo mambo”.

Young Dee alimaliza kwa kusema kama kweli maneno yanayosemwa mtaani yana ukweli basi watu watagundua haraka, “mi ambacho naweza kusema unga hauna siri haufichiki so kama mi nakula unga people they can easily notice haraka sana”.



AY " VIDEO YA BILA KUKUNJA GOT DIRECTOR ALIWEKA VITU AMBAVYO HATUKUVITARAJIA KABISA"

Ikiwa ni wiki moja imepita

tangu video iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu ya Hamis Mwinjuma aka Mwana FA na Ambwene Yessaya aka AY ya single yao ‘Bila kukunja goti’ itoke, FA amezungumzia mambo mbalimbali kuhusu video hiyo.


Kupitia kipindi cha Showtime cha Radio Free Africa ya Mwanza, FA amezungumza juu ya matarajio aliyokuwa nayo katika video hiyo na kile walichokipata baada ya kuiona video kwa mara ya kwanza.

“Always unakuwa na mawazo mengine unakuwa unafikiria kitu ambacho ungetarajia kitokee kwenye video yako kwenye wimbo wako mara nyingi, lakini that is the personal perception tu aah not necessary kile unachofikiria kitokee kitatokea, mimi binafsi nilikuwa nafikiria kitu kingine kabisa, lakini jamaa kaja na vitu vingine kabisa kama zile colors nini ah kanichanganyia habari mi naona vitu vingine ambavyo sikuvitarajia na vitu ambavyo nilikuwa navitarajia vingine havikutokea, but am all good”. Alisema FA

Upande wa gharama FA hakuwa tayari kutaja kiasi kilichotumika lakini amesema wametumia pesa nyingi ikiwa ni pamoja na kumlipia J. Martins gharama ya kumsafirisha kutoka Nigeria hadi Afika Kusini na gharama zote za kukaa siku tatu nchini humo.


“hilo ni swala ambalo tumekuwa tunajaribu kuliruka sababu gharama mara nyingi zimekuwa zinaleta matatizo lakini jua hela nyingi imetumika, imagine kama kumtoa J.Martins kutoka Nigeria kumsafirisha business class kumuweka hotel ya Michelangelo …..kwa siku tatu alizokaa yeye South Afica na vitu kama hivyo”. Aliongeza FA

FA licha ya kutopata kile alichokitarajia katika video hiyo lakini ameusifia ubora wake ambao amesema ndio kati ya sababu zilizochangia video hiyo kupitishwa na vituo vikubwa vya kimataifa kama Trace, MTV Base, na Channel O.

“moja ya vitu vimeniridhisha sana kwenye hiyo video ni quality yake achana na kila kitu kingine angalia quality yake, ndio maana imeweza zile Televisheni kubwa za muziki za Afrika zote tulizokuwa tunazilenga hiyo video imepita, kwahiyo it is a hundred percent success”.

Kama umeshaiona video ya ‘Bila kukunja goti imefanyika mazingira ya ndani (studio) FA amezungumzia sababu za kuamua kubadilisha wazo lao la mwanzo la kufanyia mtaani.

“walitupa mifano halisi wakatuambia angalia video za nje kwa mfano ukiangalia video za YMCMB na ukiangalia video za Jay Z, zote zinafanyika ndani, it’s a trend sasa hivi yani inabidi watu wafanye hivi, kuna video mbili tatu ambazo zinafanyika nje lakini trend ni kwamba video zinafanyika ndani za dunia, ndo mkondo umekuwa hivyo. Kwahiyo jamaa aka-make sense si tulikuwa tunafikiri kwamba tungeweza kufanya mtaani …..”.

Baada ya audio ya Bila kukunja goti kutoka, FA na AY walitoa mchongo kwa mashabiki wao kujirekodi style ya kucheza bila kukunja goti na ku upload clips za video hizo katika mtandao wa youtube, na kuahidi kwamba washindi wangepata nafasi ya kushiriki katika video hiyo, FA ameelezea sababu iliyokwamisha zoezi hilo.

“namna pekee ambayo tunayofikiri labda ni kuwazawadia wale ambao tunafikiri wamefanya vizuri kwenye hili , kwa sababu idea ya kutumia dancers ilishakufa wakati tunaenda South Africa kwasababu gharama na nini hatuwezi kuwasafirisha wale jamaa wanaofanya video waje kufanya hapa, that’s one lakini pia lile swala la kwamba video tunataka kuifanya ndani likawa limeondoa ile idea ya kwamba sisi tunataka dancers, watu wawe wanacheza mtaani bila kukunja goti na nini….kwahiyo tunafikiria namna ya kufanya na hizi videos, bado videos zipo na tunajua zinatudai”.

Friday, October 18, 2013

KUTOMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO NI SAWA NA KOSA LA JINAI AMBALO HUKUMU YAKE NI "KUMWAGANA"

Ndoa yoyote ambayo mke au mume hafiki kilele hiki cha Mlima Kilimanjaro…,hiyo siyo ndoa inayokwenda sawa na kuna madhara makubwa kwa pande zote, kwa maana ya mwingine kuweza kuamua kutoka. 


Ni vizuri walio kwenye ndoa kujifunza namna ya kupeana raha iwapasayo wanandoa kuipata. Kama unafikiri mkeo unaye kwa sababu amekuja kutafuta kula au kununuliwa magari na nguo, hilo ni kosa. Tafakari namna ya kupeana raha kwa kila kona.  


Kama ni kula, kila mtu anaweza kujitafutia kwa njia mbalimbali kama ni kuuza mama ntilie na kadhalika.



Mwanamke yuko kwa mume kwa sababu anahitaji kupata vitu ambavyo wanawake huvipata kutoka kwa wanaume; …Mume ndiyo kichwa, iongoze ndoa yako vizuri kwa hekima; …Kichwa kikiwa ‘bangi’, ubavu (mke) atafanya nini?



Ni suala la lazima


Kwa asili, inatakiwa mke na mume kufanikisha zoezi hilo la kuwezeshana kufika kileleni  na  ni jambo muhimu kama ilivyo kutoka jasho mwilini, maana siyo tu mwili unaondoa uchafu ndani ya mwili, pia inasaidia kuupoza mwili kuwa sawasawa.


Najua wapo wanaoweza kusema aaah mbona mimi nimekaa mwaka sitaki tena mwanaume au mwanamke na sijapata madhara… Inawezekana ni kweli, lakini wengi hupata madhara.



Kadhalika kuna wengine wanafanya vitu vya hatari kama kutumia vitu mbalimbali kama mwanasesele (sex toys) au mashine maalumu zenye umbo kama la mwanaume au wengine kujichua au kusagana.
 


Ukidumu bila tendo la ndoa muda mrefu, baadhi ya madhara madogomadogo ni kama kuwa na hasira za mara kwa mara katika mambo madogo, hii hasa kwa wanawake ambao walishawahi kuwa na uhusiano unaokaribiana kuoana au waliwahi kuwa kwenye ndoa kisha wakatoka.
 

ake huwa na hali ya kusahausahau.

Kwa wanawake, wapo ambao hutokwa damu nyingi wakati wa hedhi. Kwa watu wote yaani wanawake na wanaume hupenda kurukia mambo ya watu wengine (tabia ya kufuatilia mambo yasiyokuhusu) na wakati mwingine huongea kwa sauti ya juu hasa kunapotokea migogoro. 
 Wengine wana uwezo mkubwa wa kutukana au kutoa kauli yoyote unapomuuzi, anasema Leonard Trelawny katika jarida lake la mageuzi alilochapisha, New York Marekani.

Kwa wanaume madhara yake ni kupendelea zaidi kuangalia picha za ngono. Kwa wote kwa maana ya wanaume na wanaw

Athari nyingine ni kuumwa na kichwa kwa wanaume na wanawake, kupoteza umakini katika kazi na kwa jumla sehemu za kazi wengi wa watu ambao wamesema hawataki tena kusikia mapenzi, siyo viongozi wazuri, wana kauli chafu, hata uamuzi wao mara nyingi siyo mzuri, ingawa siyo wote.



Hali kadhalika siku ukikutana kimwili na mwenye virusi bila kinga utaambukizwa kirahisi mno. Aidha, unawaweza kuanzisha tabia nyingine mbaya kama ulevi, kukaa ofisini tu bila sababu.

NAY WA MITEGO AINGIA KUWANIA TUNZO NCHINI KENYA.

Msanii wa HipHop mwenye mashahiri yenye maneno yanayolenga mastaa tofauti tofauti nchini ambaye kwa sasa anatamba na kibao chake cha ‘Salamu Zao’ Nay wa Mitego, ameingizwa kwenye vipengele viwili kwenye tuzo zitakazofanyika nchini Kenya November 23 mwaka huu. “Thnx kwa mashabiki na media zote zina nazo sapoti muziki wangu #966. Nimeingia katika tunzo nchini kenya katika category mbili wimbo bora wa mwaka East Africa ambao ni Muziki Gani category ya pili Msanii bora wa kiume Tanzania. #966 tuombe Mungu izi zote mbili tuchukue.. Siku ya tuzo ni tarehe 23 mwezi 11..!!.”- Naywa Mitego.

Thursday, October 17, 2013

Waliodaiwa kuchoma kanisa waachiwa



MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, imewaachia huru, Hamed Sekondo na wenzie wanane waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya unyang'anyi wa kutumia silaha, kisha kulichoma moto Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Usharika wa Mbagala, baada ya kuwaona hawana kesi ya kujibu.
Uvamizi huo ulitolewa jana na Hakimu Mkazi, Waliarwande Lema, ambaye alianza kwa kuikumbusha mahakama kuwa kesi hiyo ya jinai namba 294/2012 ilikuwa imekuja kwa ajili ya mahakama kutoa uamuzi wa ama kuwaona washtakiwa wana kesi ya kujibu au la.
Akisoma uamuzi wake, Lema alisema upande wa Jamhuri katika kuthibitisha kesi yao, ulileta mashahidi 14 na kwamba awali kesi hiyo wakati inafunguliwa mahakamani hapo mwaka jana, ilikuwa na jumla ya washtakiwa 10.
Alisema kuwa hivi karibuni mshtakawa mmoja, Ramadhan Mbulu, alifariki dunia na hivyo kufanya kesi hiyo kubakiwa na washtakiwa tisa ambao kwa kipindi chote walikuwa wakiishi gerezani kwa sababu kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha lililokuwa likiwakabili halina dhamana.
Washtakiwa hao walikuwa wakitetewa na wakili wa kujitegemea, Yahya Njama.
“Baada ya kusikiliza na kuchambua ushahidi na vielelezo vilivyotolewa na upande wa Jamhuri, mahakama hii imefikia uamuzi wa kuwaona washtakiwa wote hawana kesi ya kujibu, hivyo inawaachilia huru kwa sababu upande wa Jamhuri umeshindwa kuthibitisha kesi yake,” alisema.
Lema aliongeza kuwa ushahidi wote walioutoa ni dhaifu na umeshindwa kuishawishi mahakama iwaone washtakiwa wana kesi ya kujibu.
Upande wa Jamhuri ulikuwa ukiwakilishwa na Wakili Mwandamizi, Tumain Kweka na Inspekta wa Polisi, Hamis Saidi.
Mwaka jana eneo la Mbagala jijini Dar es Salaam lilikumbwa na vurugu kubwa zilizodaiwa kufanywa na baadhi ya waumini wa Kiislamu, ambao walikuwa wakipinga dini yao kudhalilishwa kwa kukojolewa kitabu cha Kurani, hatua iliyosababisha kuchoma moto makanisa.

JWTZ wadaiwa kuchoma nyumba 100

ZAIDI ya nyumba 100 zimeteketezwa kwa moto na watu wanaodaiwa kuwa ni askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa kushirikiana na askari wa Hifadhi ya Serengeti katika vijiji vya Chegonga, Masanga na Kibasu wilayani Tarime, Mkoa wa Mara.
Inadaiwa kuwa siku hiyo ya tukio, askari wa JWTZ walitembeza vipigo kwa baadhi ya wananchi, akiwemo Diwani wa kata ya Nyanungu, Mustafa Masiani (CHADEMA), ambaye anadaiwa hali yake ni mbaya na amelazwa katika Hospitali Teule ya wilaya mjini Bunda.
Tukio hilo linadaiwa kutokea Oktoba 14, mwaka huu, ambapo wananchi hao wanadaiwa kujenga ndani ya Hifadhi ya Serengeti.
Wanajeshi hao walikuwa wamevalia sare za JWTZ wakiwa na magari sita ya serikali, walifika eneo hilo kisha kuanza kuchoma moto nyumba hizo kuanzia saa 5 asubuhi hadi saa 8 mchana.
Hatua hiyo ni utekelezaji wa operesheni ya kupambana na majangili katika hifadhi za wanyamapori, iliyotangazwa hivi karibuni na Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Hamis Kagasheki.
Baadhi ya wananchi waliozungumza na gazeti hili walisema kuwa waliochomewa nyumba zao walikuwa wakiishi nje ya mpaka wa hifadhi hiyo ambao ni Mto Mara.
“Ni kweli nyumba zaidi ya 100 zimechomwa moto na watu waliokuwa wamevalia magwanda ya JWTZ. Inavyoonekana waliochomewa hawaishi ndani ya hifadhi. Ila tunaona ni kama unyanyasaji wa raia maana hata jana kuna mtu amepigwa hadi kuuawa na askari, kwa sababu ya operesheni hii.
“Mpaka wa Tarime na Hifadhi ya Serengeti ni Mto Mara, na walikuwa wakiishi bonde la Nyanungu, ambalo serikali inadai ni eneo la hifadhi lakini wananchi tunavyoelewa si eneo la hifadhi,” alisema Chacha Heche na kuungwa mkono na Ernest Bagige mkazi wa Muriba - Tarime.
Mmoja wa viongozi wa serikali katika maeneo yaliyoathirika na tukio hilo, ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe alikiri kuchomwa kwa nyumba hizo na watu waliokuwa wamevalia sare za JWTZ, na kwamba tukio hilo limelalamikiwa na watu wengi sana.
Kwa mujibu wa kiongozi huyo, Julai 22, mwaka huu, Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Tuppa, alitembelea maeneo hayo kisha kuzungumza na wananchi hao akiwataka wahame kwa hiari yao, kwa madai kwamba eneo hilo ni Hifadhi ya Serengeti.
“Julai 22, mkuu wa mkoa alikwenda kuzungumza na wananchi waliochomewa nyumba zao majuzi. Aliwataka waondoke kwa hiari yao, lakini wananchi nao walimkatalia wakisema wanaishi nje ya hifadhi,” alisema.
Mkuu huyo wa Mkoa wa Mara, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa huo, alipotafutwa kuzungumzia tukio hilo, alisema yuko likizo mkoani Morogoro.
Alisema anachojua kuna watu walijenga ndani ya hifadhi, na kwamba kama wamekumbwa na tatizo hilo ni kwa sababu ya kuingia ndani ya hifadhi ya taifa

Watuhumiwa ugaidi wasota rumande

WATUHUMIWA 11 ambao walikamatwa wakifanya mafunzo ya kigaidi kwa kutumia CD za Al Shabaab na Al Qaeda katika msitu wa Makoloanga wilayani Nanyumbu, Mkoa wa Mtwara, jana walikwama kufikishwa mahakamani kutokana na taratibu za kuwahamishia mkoani kutokamilika.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mtwara, Zelothe Stephen, alisema kuwa wamewarudisha mahabusu wilayani Nanyumbu watuhumiwa hao.
“Leo tulitarajia kuwafikisha watuhumiwa hawa wa ugaidi katika mahakama ya wilaya, lakini kutokana na kutokamilika mazungumzo ya kuwahamishia hapa mkoani, tumekwama kuwafikisha mahakamani. Mazungumzo yatakapokamilika watarudishwa tena hapa mkoani,” alisema.
Kamanda aliwataka wananchi wawe watulivu katika kipindi hiki kwani bado uchunguzi unaendelea na mambo haya hayawezi kuisha kienyeji.
Watuhumiwa hao waliokamatwa wakifanya mafunzo ya kigaidi ni kiongozi wao, Mohamed Makande (39) mkazi wa Kijiji cha Sengenya, Hassan Omari (39) mkazi wa Kijiji cha Nalunyu na Rashid Ismail (27).
Wengine ni Abdala Yusufu (32), Salum Bakari (38), Fadhal Rajabu (20), Abbas Muhidin (32), Ismail Chande (18), Saidi Mawazo (21), Issa Abed (21) na Ramadhan Issa (26) wote wakazi wa kijiji cha Likokona, wilayani Nanyumbu.
Kundi hilo la watuhumiwa lilikamatwa na CD 25 zenye picha za mafunzo mbalimbali ya kigaidi yakiwemo ya Al Shabab, mauaji ya Osama Bin Laden, Zinduka Zanzibar, kuandaa majeshi, mauaji ya Iddi Amini na Mogadishu sniper.
Pamoja na CD hizo pia walikamata vifaa vingine ambavyo ni pamoja na DVD player moja solar panel ya watt 30, mapanga, visu, betri moja ya pikipiki, vitabu mbalimbali vya Kiislamu na tochi.
Pia walikutwa na vifaa vya kupikia na kulia vikiwemo majiko, taa, baiskeli tatu ndoo za maji, unga wa mahindi kilo 50, mbaazi kilo 50, mfuko wa kijeshi wenye nembo ya nanga ya meli yenye mistari kulia na kushoto na nyoka katikati.
Kamanda Zelothe alisema kuwa watuhumiwa hao wamefikia 13 baada ya kukamatwa wengine wawili ambao majina yao hakuyataja kwa ajili ya upelelezi zaidi.

HATIMAE MWENYE ILE SHEHENA YA MAFUVU NA VIUNGO VYA BINADAMU AJITOKEZA

There have been allegations going round that the Halloween costumes that impounded in Mombasa belonged to a very prominent politician. Former assistant minister, Omingo Magara came out to deny this allegations yesterday. Magara has however acknowledged owning some items that were in the same container with the costumes. He has given KRA and commissioner Memo 7 days to apologise for this, failure to which he’ll move to court. Meanwhile, the owners of Village Market, confirmed ownership of the items. In a press statement, the company revealed that they are to be used to decorate the Village Market during Halloween later this month. Part of the statement read, Market Masters LTD, hereby confirms that indeed we have ordered for the Halloween decorative items imported from China in container number PCIU 8125750, and are not restricted items. Just like during Easter Holiday or Christmas season, the items in question are solely used for decorating the entire shopping centre for our annual Halloween parties held within village market every last Saturday in October, for the past 17 years. We needed to replace the old worn out ones with us, in readiness for our upcoming Haloween party slated for 26th October 2013. This has put an end to the speculations that have been going round as to who owns this satanic costumes

KAULI YA ZITTO YAVIKOROGA VYAMA VYA SIASA....VYAMA VYAHAHA KUELEZA USAFI WAO

*Vyama vyahaha kuelezea usafi wa hesabu zao kabla ya kunyimwa ruzuku

KAULI ya Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe kutaka kusitishwa utoaji ruzuku kwa vyama vya siasa hadi pale hesabu zao zitakapokaguliwa, inaonekana kuwachanganya viongozi wa vyama hivyo.

Zitto alisema jijini Dar es Salaam juzi kwamba jumla ya Shilingi bilioni 67.7 zimetolewa na Serikali na kupewa vyama tisa vya siasa, lakini hadi sasa hesabu zao hazijakaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG).

Jana, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kiliibuka na kusema hesabu zao ziko makini, kwani zimekaguliwa na wakaguzi wa hesabu wa nje kwa maelekezo ya CAG.

Katibu wa Halmashauri Kuu, Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, alisema CCM imekuwa ikitekeleza utaratibu wa kukaguliwa hesabu zake tangu mwaka wa fedha 1977/78 kilipoanzishwa hadi 2003/4, ambapo hesabu zao zilikuwa zikikaguliwa na Tanzania Audit Corporation (TAC).

Alisema hesabu za chama hicho kikongwe cha siasa barani Afrika ziliendelea kukaguliwa na Januari 29 mwaka huu, CCM ilimwomba CAG awapangie mkaguzi wa hesabu za 2011/2012, CAG akawapangie kampuni ya TAC-Associates, kampuni itakayoendelea kukagua hesabu za CCM hadi 2013/2014.

“Hesabu zilizokaguliwa zote zipo kwa CAG na za 2011/2012 ziko mikononi mwa TAC-Associates, wakimaliza zitawasilishwa kwenye vikao vya chama na baadaye kwa CAG,” alisema Nape. 

Nape aliitetea CCM dhidi ya kauli ya Zitto ya kuzuia kupewa ruzuku na kwamba wapo tayari kukutana na PAC.

“Huenda kauli ya Zitto imekilenga chama chake mwenyewe kinachodaiwa kufanya matumizi mabaya ya fedha za ruzuku kwa viongozi wake kukopeshana bila kufuata utaratibu,” alisema.

Zitto ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Akizungumza na RAI kuhusu kukaguliwa kwa hesabu za CCM, Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe alionyesha kushangazwa na kauli za Nape kuhusu hesabu za chama hicho tawala.

Zitto, Mbunge wa Kigoma Kaskazini mwenye ushawishi mkubwa ndani na nje ya Chadema alisema kuwa CAG hana hesabu za CCM, na kusisitiza kuwa hakuna chama chochote kitakachopata ruzuku hadi baada ya kuwasilisha taarifa za ukaguzi wa hesabu za kipindi cha miaka minne.

“Kama CCM wanasema wamefanyiwa ukaguzi, basi hesabu zao zimekaguliwa na mkaguzi wa kichochoroni. CAG hazijui, hana taarifa za hesabu za CCM kwa kipindi cha miaka minne iliyopita.

“Hayo ni makosa, na si wao tu, bali vyama vyote vinavyochukua fedha za walipa kodi wa Tanzania na kuzitumia hovyo, havitapata tena ruzuku hizo,” alisema.

Awali, Zitto alitoa agizo hilo baada ya kamati yake kumaliza mkutano wake na Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi jijini Dar es Salaam, akisema hesabu hizo ni za kuanzia mwaka wa fedha wa 2009/10.

Vyama hivyo ni CCM, Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi, UDP, TLP, APPT Maendeleo na Chausta.

Jana Nape alimshambulia moja kwa moja Zitto kama Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, akitaka awajibike kutokana na kile alichodai kuwa ni ufujaji mkubwa wa fedha ndani ya Chadema, chama kikuu cha upinzani.

“Sote tunafahamu kuhusu kelele zilizopo mtaani juu ya matumizi mabaya ya ruzuku Chadema. Wanachama kule wanalalamika sana na kuwalaumu viongozi wao. Si ajabu hawa jamaa wakawa wanakiuka sheria hii. Zitto awashughulikie wao kwanza,” alisema Nape.

Zitto hakushitushwa na kauli hiyo ya Nape na aliliambia RAI kwamba, anachokifanya ni kutimiza wajibu wake kama Mwenyekeiti wa PAC na wala si kumkonoa yeyote ndani au nje ya Chadema.

“Vyama vyote vitakaguliwa ikiwa ni pamoja na Chadema. Ukweli utajulikana na kama kuna hatua zitachukuliwa. Si kukomoana,” alisisitiza Zitto.

Hata hivyo, RAI lilidokezwa na mwanachama mmoja wa Chadema kwamba kumekuwapo na mitafaruku ya chini kwa chini ndani ya Chadema kuhusu matumizi ya fedha, iwe za ruzuku au misaada kutoka kwa wafadhili.

Chanzo cha uhakika kutoka Makao Makuu ya Chadema, Mtaa wa Mfipa, Kinondoni ambacho ni wazi hatuwezi kukianika hadharani, kilisema kuna fedha nyingi zilizotolewa kwa ajili ya mikutano ya Vuguvugu la Mabadililo (M4C) lakini hazikutumika kama ilivyokusudiwa.

Mtoa taarifa wetu alidai kuwa posho na marupurupu ya viongozi kadhaa na wake zao ni za kutisha na kutia shaka hesabu za chama hicho hata kabla PAC haijataka kukaguliwa kwake.

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Tanzania Bara, Julius Mtatiro akizungumzia suala hilo la ukaguzi wa hesabu alisema huenda Katibu wa Bunge haijapewa taarifa sahihi kuhusu chama hicho, akidai kuwa kiliandikiwa barua ya kutakiwa kufanyiwa ukaguzi kwa sharti la kumlipa CAG.

“Ilikuwa mwaka 2011 CAG alipotuarifu kuwa kuna taasisi imeteuliwa kwa ajili ya kufanya ukaguzi, tukauliza inakuwaje kazi inayofanyika ni ya Serikali sisi tumlipe mkaguzi?

“Hofu yetu ilikuwa kwamba tungeweza kutuhumiwa kumuhonga mkaguzi huyo. Sasa huenda Zitto hajapewa taarifa sahihi kabisa,” alisema Mtatiro. 

Kwa mujibu wa sheria, CAG analo fungu lake kwa ajili ya kufanya ukaguzi na kamwe hapaswi kulipwa na mteja anayekaguliwa.


Wadadisi wa mambo wanasubiri kwa hamu kuona ninikitatokea ndani ya vyama hivyo vikubwa vya siasa nchini; CCM, Chadema na CUF kama vikishindwa kuhalalisha matumizi ya fedha za ruzuku walizopewa.

MCHUNGAJI ADAI KUWAUA KANUMBA NA SHARO MILIONEA, AELEZEA JINSI ALIVYOFANYA....WAUMINI WAPIGWA NA BUTWAA

Mchungaji Mayanga (mwenye kipaza sauti) akitoa ushuhuda. Mwanaume aliyetambulishwa kwa jina la Mchungaji Mayanga amewashangaza waumini baada ya kudai kanisani kuwa yeye ndiye aliyewaua mastaa wawili Bongo, Hussein Ramadhan Mkiety ‘Sharo Milionea’ naSteven Kanumba ‘The Great’. Tukio hilo lilitokea Jumapili iliyopita ya Oktoba 13, mwaka huu, huko Mzambarauni, Mbagala-Charambe jijini Dar katika Kanisa la Powerful Gospel Ministry lilipo chini ya Mchungaji Meshak Punkanya ambapo Mayanga alipewa nafasi ya kutoa ushuhuda. VIFO MILIONI 605 Mchungaji huyo alielezea kujuta kwake mbele ya kanisa kwa kudai kuwa kabla ya kuokoka alikuwa mchawi mkubwa aliyeishi kuzimu na kufanya kazi za mauaji sambamba na shetani mkuu (Lusifa) kwa kuwatumia vibaraka wake na majini. Mchungaji Mayanga alikiri kutekeleza vifo vya watu wapatao milioni 605 wakiwemo waigizaji hao
Steven Kanumba. WAMO FIVE STARS, MTOTO WA DANDU Alisema kuwa kati ya watu aliowaua kwa njia za kishirikina wamo waimbaji wa Taarab wa Kundi la Five Stars wapatao 14, Kanumba, Sharo Milionea na mwanamuziki James Dandu ‘Mtoto wa Dandu’. Pia alidai kuwa alihusika katika vita kati ya aliyekuwa Rais wa Iraq, Sadam Hussein na Marekani kwa kutumia pepo la uchonganishi alilolitaja kwa jina la ‘Magweju’. Pia mchungaji huyo alidai kuhusika na shambulio la hivi karibuni la Al-Shabaab katika maduka ya Westgate la Nairobi nchini Kenya na matukio mengine mengi hadi kufikia idadi hiyo ya vifo vya watu milioni 605.
Hussein Ramadhan Mkiety ‘Sharo Milionea’. AWAONEA HURUMA WASANII, AWAONYA Mchungaji huyo aliendelea kusimulia kuwa alipokuwa katika ulimwengu wa giza aliwahi kuwaonea huruma wasanii kama Kanumba, Sharo Milionea na Mtoto wa Dandu na kuwatokea kimiujiza akiwaonya waokoke kabla ya kuchukua roho zao huku mashabiki wao wakibaki na simanzi wakiamini kuwa vifo vyao ni vya kawaida. Alidai kuwa baada ya kuwafuata mastaa hao na kuwaonya walikataa na badala yake akawaua. Akiendelea kulishuhudia kanisa, Mchungaji Mayanga alisema kuwa kwa sasa ameokoka na kuachana na mambo ya giza, hivyo haogopi kuzungumza ukweli kwa kuwa roho wa Bwana anamuongoza kushuhudia kila kitu alichokifanya ili waumini watambue uwezo wa Mungu.
Gari la Sharo baada ya ajali. ANA SIRI NZITO ZA VIGOGO Huku akiomba hifadhi ya majina ya wahusika, mchungaji huyo alihitimisha ushuhuda wake kwa kudai kuwa ana siri nzito za vigogo au watu wakubwa ambao aliwahi kwa namna moja au nyingine kuwapa utajiri wa nguvu za giza. UTABIRI Hata hivyo, baadaye jamaa huyo alijitabiria kuwa atakamatwa na kufungwa siku moja kutokana na siri alizonazo. “Yaani nina siri za watu wengi sana, nikiwaambia mtaogopa na nchi itatikisika. Najua siku moja watu watanikamata na kunifunga pingu kwa siri nilizonazo, lakini kamwe siogopi kwa kuwa Bwana ananiongoza,” alisema Mchungaji Mayanga.
Jeneza la Kanumba. KANUMBA, SHARO MILIONEA Kanumba alifariki dunia mwaka jana akiwa nyumbani kwake Sinza-Vatican, Dar huku Sharo Milionea akipoteza uhai kwenye ajali ya gari iliyotokea wilayani Muheza, Tanga wakati msanii huyo akienda kwao mkoani humo akitokea Dar.

CHEKI VIDEO MPYA YA KABINTI SPECIAL YA DULLY SYKES

TAZAMA VIDEO INAYOONESHA MAGAIDI WALIVYO KUWA WAKILANDA LANDA NDANI YA WASTEGATE,MMOJA AKIWEKA SILAHA CHINI NA KUPIGA DUA.

Wednesday, October 16, 2013

Ney wa Mitego: Mlinzi wangu ni Mungu

MKALI wa muziki wa hip hop nchini, Emmanuel Elibariki ‘Ney wa Mitego’ amesema mlinzi wake ni Mungu na hana muda wa kutafuta wa kumlinda au kuhangaika kwa waganga wa kienyeji. Kauli hiyo imekuja baada ya kusemekana kwamba, kuna wasanii ambao walisafiri kwenda mkoani Tanga kwa ajili ya kumroga msanii huyo ili apunguze kasi ya kuimba na kuacha kuwataja watu mbalimbali katika nyimbo zake. Akizungumza katika mahojiano na Clouds FM, Ney alisema, alipigiwa simu na mganga huyo na kuelezwa kwamba, kuna watu ambao walifika kwake na kumtaka yeye amtumie radi au amfanye apoze viungo vya mwili kutokana na kuwaimba katika baadhi ya nyimbo zake. “Kwa maana hiyo, hao watu walitaka kuniua, lakini nilipomuuliza mganga huyo kwamba ni kina nani, alisema hawezi kuniambia moja kwa moja mpaka atakapopata ruhusa ya kunitajia kutoka kwa mizimu yake kama alivyopewa ruhusa ya kuniambia,” alisema Ney na kuongeza: “Mimi siogopi lolote, sina haja ya kutafuta ‘bodigadi’ wala askari wa kunilinda, mlinzi wangu ni Mungu na najiamini sina haja ya kuogopa lolote, hao watu wanajisumbua tu, kama wao ni wasanii kwanini wasifanye kazi nzuri kila mmoja azione?” Nyimbo ambazo Ney wa Mitego ametaja baadhi ya majina ya watu ndani yake ni ‘Salamu Zao’ na ‘Nasema Nao’.

KENDRIC LAMAR ASHINDA TUZO 5,KWENYE TUZO ZA BET HIPHOP,SOMA ORODHA YA WASHINDI WOTE.

Rapa ambaye mimi binafsi namkubali kinoma Kendric Lamar ameongoza kwa kuchukua Tuzo 5 katika Tuzo za Hip Hop za BET mwaka 2013.Kendric Lamar ameshinda tuzo kubwa ikiwemo Album bora ya mwaka ' ‘Good Kid,m.A.A.d City' na 'Lyricist of the year' yaani mwandishi bora wa mashairi'.Aliyefatia kwa kuondoka na tuzo nyingi zilizoonyeshwa jana ni Drake ambaye ameondoka na tuzo 4. LIST NZIMA YA WASHINDI; Best Hip-Hop Video WINNER: Drake- "Started From the Bottom" A$AP Rocky (featuring Drake, 2 Chainz and Kendrick Lamar) - "F---in' Problems" B.o.B (feat. T.I. and Juicy J) - "We Still in This" J. Cole (feat. Miguel) - "Power Trip" Kendrick Lamar - "Bitch, Don't Kill My Vibe" Best Collabo, Duo or Group WINNER: A$AP Rocky (feat. Drake, 2 Chainz and Kendrick Lamar) - "F---in' Problems" Ace Hood (feat. Rick Ross and Future) - "Bugatti" J. Cole (feat. Miguel) - "Power Trip" French Montana (feat. Rick Ross, Drake and Lil Wayne) - "Pop That" Kendrick Lamar (feat. Drake) - "Poetic Justice" Wale (feat. Tiara Thomas) - "Bad" Best Live Performer WINNER: Jay Z 2 Chainz J. Cole Kendrick Lamar Kanye West Lyricist of the Year WINNER: Kendrick Lamar J. Cole Drake Jay Z Wale Video Director of the Year WINNER: Benny Boom A$AP Ferg and Scout Director X Dre Films Hype Williams Hustler of the Year WINNER: Jay Z Diddy Kendrick Lamar T.I. Kanye West Best Hip-Hop Style WINNER: A$AP Rocky WINNER: Nicki Minaj 2 Chainz Kendrick Lamar Kanye West Best Hip Hop Online Site WINNER: World Star Hip-Hop All Hip-Hop Complex Global Grind Rap Radar Best Club Banger WINNER: French Montana (feat. Rick Ross, Drake and Lil Wayne) - "Pop That" Ace Hood (feat. Rick Ross and Future) - "Bugatti" A$AP Rocky (feat. Drake, 2 Chainz and Kendrick Lamar) - "F---in' Problems" Drake - "Started From the Bottom" Trinidad Jame$ - "All Gold Everything" Album of the Year WINNER: Kendrick Lamar - good kid, m.A.A.d city J. Cole - Born Sinner Jay Z - Magna Carta... Holy Grail Nas - Life is Good Wale- The Gifted Sweet 16 WINNER: Kendrick Lamar - "F---in' Problems" Diddy - "Same Damn Time (Remix)" Drake - "Versace (Remix)" Future - "Bugatti" Wiz Khalifa - "U.O.E.N.O. (Remix)" Impact Track WINNER: J. Cole (feat. TLC) - "Crooked Smile" Jay Z (feat. Justin Timberlake) - "Holy Grail" Macklemore and Ryan Lewis (feat. Mary Lambert) - "Same Love" Wale (feat. Sam Dew) - "LoveHate Thing" Kanye West - "BLKKK SKKKN HEAD" MVP of the Year WINNER: Kendrick Lamar 2 Chainz Drake Jay Z J. Cole Track of the Year WINNER: Drake - "Started From the Bottom" J. Cole (feat. Miguel)- "Power Trip" A$AP Rocky (feat. Drake, 2 Chainz and Kendrick Lamar) - "F---in' Problems" Kendrick Lamar - "Bitch, Don't Kill My Vibe" Ace Hood (feat. Rick Ross and Future) - "Bugatti" Producer of the Year WINNER: Mike Will Made It J. Cole Hit-Boy DJ Mustard Pharrell Williams DJ of the Year WINNER: DJ Drama DJ Envy Funkmaster Flex DJ Khaled DJ Scream Best Mixtape WINNER: Big Sean - Detroit Chance the Rapper - Acid Rap Travi$ Scott - Owl Pharaoh Stalley - Honest Cowboy Trinidad James - Don't be S.A.F.E. Rookie of the Year WINNER: A$AP Ferg Action Bronson Earl Sweatshirt Joey Bada$$ Trinidad James Best Hip Hop Online Site WINNER: World Star Hip-Hop All Hip-Hop Complex Global Grind Rap Radar People's Champ Award WINNER: Drake - "Started From the Bottom" Macklemore and Ryan Lewis (feat, Ray Dalton)- "Can't Hold Us" A$AP Rocky (feat. Drake, 2 Chainz and Kendrick Lamar) - "F---in' Problems" Kendrick Lamar - "Bitch, Don't Kill My Vibe" J. Cole (featuring Miguel) - "Power Trip"

Juacali featuring Jovial - Jiachilie (Official video)

Rais Kikwete akiwa na viongozi wa vyama pinzani.

Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Vyama vya upinzani na wasaidizi wao waandamizi muda mfupi kabla ya kuanza mazungumzo kuhusu rasimu ya katika ikulu jijini Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto mbele Isaack Cheyo UDP, James Mbatia NCCR Mageuzi, Professa Ibrahim Lipumba CUF, Freeman Mbowe CHADEMA, Philip Mangula CCM, na Bibi Nancy Mrikaria aliyemwakilisha Mwenyekiti wa TLP Mhe.Agustine Lyatonga Mrema.Waliosimama Nyuma kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu CUF Bwana Julius Mtatiro,Mhe. Tundu Lissu CHADEMA, Bwana Martin Mng’ong’o NCCR Mageuzi ,Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu na Bunge William Lukuvi, Mhe.Habib Mnyaa CUF, Mbunge wa Ubungo Kwa tiketi ya CHADEMA Mhe.John Mnyika, Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu Mhe.Steven Wassira na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Mathias Chikawe. (picha zote: Freddy Maro/IKULU).


TAARIFA KWA UMMA KUTOKA KURUGENZI YA MAWASILIANO IKULU


MKUTANO kati ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wa vyama vya siasa vyenye uwakilishi Bungeni umemalizika Ikulu, Dar Es Salaam, muda mfupi uliopita leo, Jumanne, Oktoba 15, 2013 kwa pande hizo mbili kukubaliana kama ifuatavyo:

Moja , kwamba vyama vyote vya siasa nchini vyenye mawazo, maoni na mapendekezo ya kuboresha Sheria ya Kurekebisha 
Sheria ya Mabadiliko ya Katiba viwasilishe mapendekezo yao haraka Serikalini ili ifatutwe namna ya kuyashirikisha mapendekezo hayo katika marekebisho ya Sheria hiyo.

Pili, kwamba vyama vya siasa nchini, kama wadau muhimu katika mchakato wa Katiba Mpya, viangalie namna ya kukutana na kujenga mfumo wa mawasiliano na maridhiano wa jinsi kwa pamoja vitakavyosukuma mbele mchakato huo kwa maslahi mapana ya nchi yao na mustakabali wa taifa. Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) kimepewa jukumu la kuratibu jambo hilo ikiwa ni pamoja na kuandaa mkutano wa vyama hivyo na wadau wengine nchini.

Viongozi wa vyama vyama vya siasa waliokutana na Mheshimiwa Rais Kikwete ni Mheshimiwa Profesa Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa CUF; Mheshimiwa Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CHADEMA na Mheshimiwa James Mbatia ambaye ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi.

Wengine ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Mheshimiwa Philip Mangula, Mheshimiwa Isaack Cheyo ambaye amemwakilisha Mwenyekiti wa Chama cha UDP Mheshimiwa John Cheyo na Mheshimiwa Nancy Mrikaria ambaye amemwakilisha Mwenyekiti wa TLP Mheshimiwa Augustine Mrema. Waheshimiwa John Cheyo na Mrema wako nje ya nchi.

Wengine ambao wameambatana na wenyeviti wao ni Mheshimiwa H. Mnyaa na Bwana Julius Mtatiro wa CUF, Waheshimiwa Tundu Lissu na John Mnyika wa CHADEMA na Bwana Martin Mng’ongo wa NCCR-Mageuzi.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

Hasara ya mtoto kuzaa mtoto: Mtoto wa miaka minne apigwa vibaya na kufa

Hapa jijini Phoenix, mzazi mmoja (mama) na rafiki yake wa kiume wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kusababisha kifo cha mtoto wa miaka minne.

Msemaji wa Polisi bwana James Holmes amesema maofisa waliofika nyumbani kwa wawili hao juzi, siku ya Jumapili, punde baada ya mama huyo alipopiga simu ya dharura ya 911 kutoa taarifa ya kuomba msaada, walimkuta mtoto hapumui.

Mama huyo ambaye ni kijana wa miaka 19, Melissa Centeno alisema mwanaye alipigwa tumboni usiku wa Ijumaa na
 baada ya hapo akaanza kulalamika maumivu ya tumbo.

Rafiki wa Mellisa mwenye umri wa miaka 22, Sergio Ortiz amewambia maafisa kuwa alimchapa marehemu binti huyo mwishoni mwa juma hadi akaanguka kwenye karo la kuogea na kuchubuka usoni.  Lakini, maofisa waliofanya uchunguzi wamesema kuwa sehemu na idadi ya michubuko katika mwili wa marehemu haiendani na maelezo ya watuhumiwa.

Sasa hivi wapo mikononi mwa polisi wakisubiri kusomewa mashitaka  baada ya vipimo vya kitaalamu kufanyika.

Kisa hiki kinasikitisha mno kwani waliotenda kosa nao ni miaka michache tu walivuka umri wa utoto. Ikiwa Melissa ana umri wa miaka 19 kwa sasa, ina maana alimzaa mwanaye akiwa na umri wa miaka 15 hivi. Rafiki yake wa kiume (ambaye si baba mtoto) ana miaka 22. Nadhani huenda hawa hakuwa wamepevuka kiasi cha kutosha kubeba majukumu ya uzazi na malezi bora, ikizingatiwa kuwa  wanaishi kaitka jamii ambayo mtoto akishavuka umri wa miaka 18, kisheria --ikiwa kila kitu kipo sawa-- anakuwa na haki ya kufanya maamuzi yake bila kuingiliwa na mzazi (ikiwa ni pamoja nahaki ya mwanaye, labda wazazi au au mzazi mwenza athibitishe kwa vielelezo kuhusu mapungufu ya mama huyo kumtunza mjukuu/mtoto) na kwenye mfumo wa maisha ambapo kila mtu anajijali kivyake (mind your own business, everybody for themselves and God for us all).

Jukumu la wazazi na walezi kuwa waangalizi au jamii kama kijiji kusaidiana kulea na kumkuza mtoto ni dhana iliyosahaulika kwa nyakati hizi ambazo mtoto ni mali ya Serikali na mwanangu ni wangu, ole wako umguse!

Hiki si kisa cha kwanza, na si kigeni lakini kutokana na visa hivi kujirudia, nimewaza na kutafakari nilivyolelewa na kujiuliza endapo si kwa jitihada na ushirikiano wa familia na wanakijiji, ningekuwa wapi? Wazazi wetu walikosea? Kama ndiyo, sisi tunarekebishaje? Kama siyo, kwa nini tumeupa kisogo utamaduni wa "It takes a village to raise a child"?

Jux - Uzuri Wako.(Official Video)

Monday, October 14, 2013

Auawa akimwokoa baba yake

MFANYABIASHARA maarufu katika mji mdogo wa Galapo, wilayani Babati, Mkoa wa Manyara, Walter Kanda (31), ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wanaosadikiwa kuwa majambazi alipokwenda kumuokoa baba yake, John Kanda (62), aliyevamiwa nyumbani kwake.
Katika uvamizi huo licha ya kumuua mfanyabiashara huyo, watu hao pia waliiba vitu mbalimbali ikiwa ni pamoja na bunduki aina ya Rifle iliyokuwa ikimilikiwa na Kanda na kutokomea nayo.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda ya Polisi Mkoa wa Manyara, Akili Mpwapwa, alisema uchunguzi unaendelea kuhusiana na tukio hilo ili kuwabaini wahusika kama hawana mahusiano na majangili wanaotafutwa.
“Tukio la mauaji ni tukio kubwa na linahitaji uchunguzi makini ili kujiridhisha na wote wanaotuhumiwa kabla ya hatua nyingine za kisheria kufuatwa kwani mbali na mauaji hayo kuna silaha imeibwa, pia kuna migogoro ya mashamba, lakini kule pia yapo matukio ya uwindaji haramu, hivyo inahitaji uchunguzi wa kina kujiridhisha,” alisema Mpwapwa.
Habari za ndani zinasema kuwa tayari kuna watu kadhaa wanashikiliwa kuhusiana na tukio hilo akiwamo Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Endadoshi, Kata ya Qash, Luka Bunye (CCM)  kwa tuhuma za kuhusika katika tukio hilo.
Pamoja na mwenyekiti huyo pia wapo wakulima wenzake, Everest Joachim, mkazi wa Kijiji cha Halah  na Jumanne Manja wa Qash Mwisho.
Kamanda huyo alisema tukio hilo lilitokea Oktoba 8, mwaka huu, saa 5:30 usiku.
Habari zaidi zimeeleza kuwa kabla ya tukio hilo, Kanda (62), ambaye ni baba yake marehemu alitoka ndani kwenda chooni na ghafka alikutana na kundi la watu waliomrushia risasi kwa kutumia silaha inayosadikiwa kuwa ni bastola huku wengine wakimkata mapanga.
“Risasi hiyo ilipiga ukuta wa choo, nikamrukia mmoja nikawa najikinga naye ili yule mwenye bastola asinipige, tukaburuzana hadi mlango wa choo. Nikamsukumia kwa wenzake, nikapata nafasi nikaingia chooni na kufunga mlango,” alisema.
Aliongeza kuwa baada ya kuingia chooni, watu hao walianza kusukuma mlango huku akipiga kelele za kuomba msaada, ghafla mtoto wake alitoka nje na kuwatambua wale watu ndipo walipompiga risasi ya ubavuni na kuanguka.
“Watu hao waliingia ndani na kuchukua bunduki yangu aina ya Riffle, fedha na nyaraka zinazohusu mashamba yangu, ambapo tayari majirani walikuwa wameanza kutupa mawe juu ya nyumba yangu, hivyo wakakimbia kusikojulikana,” alisisitiza.
Eneo hilo limegubikwa na migogoro ya mashamba kwa muda mrefu, inayosababisha hofu baina ya wakazi wa maeneo hayo.

Ufoo: Sijambo, naendelea vizuri

Kaka wa marehemu Anthery Mushi aliyemuua mkwewe, kumjeruhi mzazi mwenzake, Ufoo Saro na kujipiga risasi, Silva Andrea akizungumza jijini Dar es Salaam jana, kuhusu taratibu za mazishi ya mdogo wake anayetarajiwa kuzikwa wiki hii, Uru, Moshi Vijijini mkoani Kilimanjaro. Wa pili kushoto ni kaka mwingine wa marehemu, Isaya Mushi.Picha na Michael Jamson



Dar es Salaam. Hali ya mwandishi wa habari wa Kituo cha Televisheni cha ITV, Ufoo Saro aliyejeruhiwa vibaya baada ya kupigwa risasi mbili juzi huko Kibamba, Dar es Salaam inazidi kuimarika na jana alizungumza na blog hili na kusema; “Sijambo, naendelea vizuri.” Ufoo, ambaye amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, hata hivyo, anazungumza kwa shida kutokana na kukabiliwa na maumivu baada ya kufanyiwa upasuaji juzi. Mwandishi huyo amehamishiwa katika wodi ya upasuaji wa moyo huku kiongozi wa wodi hiyo, ambaye alikataa jina lake kuandikwa gazetini, akieleza kuwa walimhamishia huko ili apate muda zaidi wa kupumzika. “Watu wanakuja kwa wingi kumjulia hali, tuliona tumhamishe ili apumzike,” alisema kiongozi huyo. Kabla ya kupelekwa katika wodi hiyo, Ufoo alikuwa katika wodi ya Kibasila na baadaye alihamishiwa katika Chumba cha Wagonjwa Wanaohitaji Uangalizi Maalumu (ICU). Ufoo alipigwa risasi na mzazi mwenzake, Anthery Mushi ambaye alijiua baadaye. Pia Mushi anatuhumiwa kumuua mama yake Ufoo, Anastazia Saro wakati wa tukio hilo. Mazishi ya mama yake Ufoo yamepangwa kufanyika Ijumaa huko Machame mkoani Kilimanjaro. Ufoo aongea kwa shida Mara baada ya mwandishi wa gazeti hili jana kuingia katika chumba alicholazwa Ufoo huku akisindikizwa na wauguzi watatu, mwandishi huyo alitoa mkono wake na kusema; “Njoo hapa unisalimie huku umenishika mkono.” Huku akionyesha uchovu na kusikia maumivu, alizungumza kwa tabu na kusema; “Sijambo naendelea vizuri.” Mara baada ya wauguzi hao kumweleza kuwa kati ya waandishi zaidi ya 30 waliofika kumjulia hali ni watatu tu ndiyo walioruhusiwa kumwona alitaka kujua ni kina nani waliobaki nje kwa kuhoji; “Nani hao wako nje.”