HABARI MOTO MOTO ...
Monday, October 7, 2013
kauli ya Rais JK juu ya vyama vya upinzani.
Kufuatia mvutano uliozuka baina ya serikali na vyama vya upinzani nchini Tanzania ,Rais Jakaya Kikwete wa nchi hiyo amevitaka vyama vya kisiasa visiitishe maandamano vilivyopanga na kuwa yuko tayari kuzungumza na vyama hivyo.Mvutano huo uliibuka baada ya vyama hivyo kutoka bungeni hivi karibuni, vikidai kwamba baadhi ya vifungu vya rasimu ya Katiba iliowasilishwa bungeni vilibadilishwa. Muungano wa vyama vya upinzani vikiwemo Chadema, CUF , NCCR-Mageuzi na UPDP uliitisha maandamano nchini kote kumshinikiza Rais Kikwete kutosaini rasimu hiyo. Jee Tanzania itafanikiwa kweli kuwa na katiba itakayokubalika kabla ya uchaguzi mkuu ujao 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment