HABARI MOTO MOTO ...

Friday, October 11, 2013

P - Square kupagawisha Dar

KUNDI la wasanii nyota duniani la P-Square kutoka Nigeria linatarajiwa kufanya onesho kubwa jijini Dar es Salaam, Novemba 23. Kundi hilo linaongozwa na wasanii mapacha, Peter na Poul Okoye. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mratibu wa ziara hiyo kutoka kituo cha runinga cha East Africa (EATV), Hillary Daudi, ‘Zembwela’, alisema, taratibu zote muhimu za ziara hiyo zimekamilika. Zembwela aliongeza kuwa kundi hilo litakuja na wasanii 13, ambao watapiga shoo ya kihistoria katika medani ya muziki wa kizazi kipya hapa nchini. “Lengo kubwa la kuwaleta wanamuziki hawa wanaoongoza kwa umaarufu kila kona duniani, kwanza ni kutoa burudani, lakini kingine kikubwa ni kuja kutoa somo kwa wanamuziki wetu hapa nchini, namna ambavyo muziki unaweza kufanyika katika hali tofauti na walivyozoea,” alisema Zembwela. Akizungumzia ziara hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Udhamini wa Vodacom Tanzania, Calvin Twissa, wao kama wadhamini wanajipanga kutoa tiketi za bure, hivyo kazi kwa watumiaji wa Vodacom, kwani watatangaziwa namna ya kuzipata na kwenda kuwashuhudia vijana hao machachari. “Vodacom tunajivunia kuleta kundi hili la wanamuziki wenye jina kubwa duniani, mtakumbuka juzi tulisaini mkataba mnono na Naseeb Abdul ‘Diamond’, kupitia kibao chake cha ‘My Number One’, hivyo tunaahidi kufanya kazi na wasanii wengine wengi wa hapa nyumbani,” alisema Twissa

No comments:

Post a Comment