KUFUATIA
mgogoro uliopo kati ya Serikali na wamiliki wa maroli nchini, mafuta ya Petrol
na mafuta ya taa, yameanza kuadimika Jijini hapa. Imebainika.
Kikosi kazi cha mtandao wa www.geofreymtenzi.blogspot.com jana, lilitembelea baadhi ya vituo vya mafuta Jijini Mbeya na nje ya Jiji,
na kuelezwa kuwa mgomo huo ukiendelea, huduma hiyo itasitishwa baada ya vituo
hivyo kuishiwa mafuta kutokana na magari kutosafirisha bidhaa hiyo.
Baadhi ya
wamiliki na wauzaji wa mafuta hayo, ambao waliomba hifadhi ya majina yao,
walisema kuwa, madai yao ni ya msingi na kamati ya bunge ya miundombinu
inayajua na ilikwisha yatolea maamuzi.
‘’Tunamshangaa
Waziri Magufuli, tunajua anapata pasenti kupitia maamuzi yake kutoka kwa
wakandarasi wa barabara na ndiyo maana anapuuza hata maagizo ya kamati ya
Miundombinu iliyoketi Mjini Dodoma April 29, mwaka huu’’ walisema.
Moja ya
barua ambayo aliandikiwa Mwenyekiti wa Tatoa May 16, mwaka huu, ambayo G MTENZI BLOG imeiona nakala yake, imesema kuwa, Tanroad wanafanya kazi kwa mazoea na
uzembe .
‘’Jambo
ambalo linaleta usumbufu na ucheleweshaji kwenye kusafirisha mizigo ya wateja
na hivyo kuwa sababu ya wateja kukimbia kupitisha bidhaa bandari ya Dar es
Salaam’’ imesema barua hiyo.
Sanjari na
hayo, barua hiyo ambayo nakala yake ilipelekwa kwa Waziri wa Ujenzi na
kupokelewa May 17, mwaka huu, Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Tanroad Makao makuu
na Tanroad Mkoa wa Dar es Salaam ikilalamikia suala la mizani.
Imeelezwa
kuwa, mizani zinazotumika kupima magari yanayobeba mizigo mizito na abiria nchi
Tanzania, zina mapungufu makubwa ambayo yanadhaniwa kuwa ni makusudi ya
watendaji wa mizani hizo ili kujipatia fedha.
Mfano katika
Mizani ya Kibaha May 11,05,2013, Mzigo uliopimwa na kupatikana na uzito wa Kgs
44.850, mizani ya Mikese ulipatikana na Kgs 39.900 na Kihonda Kgs 35.250 na
hiyo ni gari hiyo hiyo moja.
Katika gari
hiyo hiyo, siku iliyofuata katika Mizani ya Dodoma zilipatikana Kgs 46.759, mizani
ya Singida ilikuta gari hiyo ikiwa na Kgs 38.600, Tinde Kgs 44.700 na Usagara
Kgs 45.320.
Sanjari na
hayo, taarifa iliyonukuliwa kutoka kwenye hotuba ya kambi ya upinzani. Sehemu
hii inaonyesha ubadhirifu wa fedha kwenye wizara iliyoko chini ya Dr John Pombe
Magufuli.
Mheshimiwa
Spika,baada ya fedha hizi kupunguzwa kiasi cha shilingi bilioni 95 na kupelekwa
wizara ya uchukuzi zilibakia kiasi cha shilingi bilioni 252.975.
Katika
kifungu hiki, leo tumelazimika kulikumbusha Bunge kuhusiana na suala hili kwani
kwa mujibu wa ripoti ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ya mwaka
husika wa fedha kuhusiana na kifungu hiki alisema, naomba kunukuu
“malipo ya
madeni ya mwaka wa nyuma yaliyolipwa kwa fedha za 2011/2012 kwa kutumia jina la
mradi usiohalisi Tshs.252,975,000,000.
Miradi
katika wizara ilipewa namba 4168 kwa ajili ya kupitisha malipo ya madeni ya
miaka ya nyuma kwa miradi inayotekelezwa na TANROADS. Namba hii sio halisi''
No comments:
Post a Comment