MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Profesa Mwesiga Baregu, amefichua siri ya madai ya usaliti ndani ya chama hicho.
Akizungumza na Mtanzania katika mahojiano maalumu yaliyofanyika jijini Dar es Salaam wiki hii, Profesa Baregu alisema kiini cha tuhuma na madai ya usaliti ndani ya Chadema ni kutoaminiana na kukosekana kwa uvumilivu.
Alisema kitendo cha wanachama na viongozi kunyoosheana vidole vya usaliti kinakiangusha chama na kwamba Chadema kimefeli katika mambo matatu, ambayo ndiyo yanapaswa kuwa msingi wa chama na kama yangezingatiwa mapema, hoja ya usaliti isingezungumzwa leo.
Aliyataja mambo hayo yanayozalisha hoja nzito ya usaliti iliyosababisha baadhi ya wanachama wa chama hicho kuvuliwa uanachama kuwa ni kusikilizana, kuvumiliana na kuaminiana.
“Kukosekana kwa mambo hayo ndio kiini cha kuibuka kwa hoja ya usaliti, hatua hii ni mbaya katika maendeleo ya chama kinachojijengea uaminifu kwa wananchi,” alisema.
HABARI MOTO MOTO ...
Monday, January 27, 2014
Sunday, January 26, 2014
Mfuko wa Rais wakumbwa na kashfa
Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (PTF) umekumbwa na kashfa nyingine
baada ya kudaiwa kuwadhulumu wanachama wake akiba zenye thamani ya zaidi
ya milioni 10/-.
Wanachama hao ambao ni kikundi cha Mbezi A na B wamedai kuwa mpaka
sasa imeshapita miaka mitatu wamekuwa wakipigwa kalenda kila wakati kuwa
watapatiwa akiba zao jambo ambalo limeshindikana kutekelezeka.
Saturday, January 25, 2014
Mwanamke wa miaka 48 , mkazi wa Rombo akamatwa na polisi kwa kufanya ngono na watoto wa miaka 9- 14 kwa zamu.....
Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Aretas Joseph, (48), mkazi wa kijiji cha Lesoroma tarafa ya Useri, wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro, amehojiwa na polisi mkoani hapa kwa tuhuma za kufanya mapenzi na watoto wadogo wa kiume, wenye umri kati ya miaka 9 na miaka 14, jambo linaloelezwa kuwa ni shambulizi la aibu.
KASHFA YA KUSAGANA KATI YA IRENE UWOYA NA MARIAM....YAWA GUMZO MITANDAONI UKWELI HUU HAPA..
Mariam IsmailMastaa wa filamu nchini Mariam Ismail na Irene Uwoya wanadaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi(usagaji) na kudaiwa kuishi pamoja kabisa. wiki kadhaa nyuma muigizaji mmoja chipukizi anayekuja juu kwa kasi aliutonya mtandao huu kwa kusema " Mariam Ismail na Uwoya wanasagana tena wanaishi pamoja kabisa, fuatilieni mtajua".
Subscribe to:
Posts (Atom)


