HABARI MOTO MOTO ...

Friday, May 2, 2014

`Serikali iunge mkono mpango wa kupunguza athari dawa za kulevya`


Serikali imetakiwa kutekeleza na kuunga mkono mpango wa kupunguza madhara hasi yanayohusiana na matumizi ya dawa za kulevya pamoja na kurejesha maisha bora katika jamii. Hayo yalisemwa Dar es Salaam na Greg Denham, Mratibu katika Mtandao wa Kimataifa wa Utekelezaji Sheria na VVU (LEAHN) alipotembelea Mtandao wa Watu wanaotumia dawa ya kulevya nchini (TaNPUD) na Ofisi za Madakitari wa Ulimwengu (MdM).